Yared wa Ethiopia

Mt. Yared alivyochorwa karne ya 15.

Yared wa Ethiopia (kwa Kige'ez: ቅዱስ ያሬድ; 25 Aprili 505 - 20 Mei 571[1][2]) ni kati ya Wakristo maarufu wa Ethiopia[3].

Aliishi katika Ufalme wa Axum katika karne ya 6. Anatajwa kama mtunzi na mwanzilishi wa muziki wa Kikristo nchini, muziki wa utamaduni wa Ethiopia na wa Eritrea. Alikuza muziki wa kidini wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia, na matumizi katika muziki wa liturujia, pamoja na mfumo wa nota wa Ethiopia. Zaidi ya hayo, alitunga Zema, au mapokeo ya nyimbo za Ethiopia-Eritrea, ambazo zinaimbwa hadi leo.[4]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Mei.

  1. Chavis, Charles L. (2011-04-05). "Yared (Saint), 505-571 AD" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-05-03.
  2. Giday, Belai (1991). Ethiopian Civilization (kwa Kiingereza). B. Giday.
  3. https://dacb.org/stories/ethiopia/yared/
  4. "Saint Yared (505-571) •" (kwa American English). 2011-04-05. Iliwekwa mnamo 2023-02-26.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search